Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 20:40

Uchunguzi wabaini maafisa polisi 2,000 Kenya wana matatizo ya kiakili


FILE -May 16, 2016, Afisa wa kikosi cha kuzuia ghasia akirejea kumpiga mateke mwandamanaji aliyeanguka chini wakati akijaribu kuwakimbia wakati wa maandamano mjini Nairobi, Kenya. Tukio hilo lililaaniwa na Wakenya na wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kenya na Marekani

Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai Jumanne aliuambia mkutano wa maaskofu na viongozi wa juu wa dini kwamba wamegundua idadi ya kushangaza ya kesi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu kwa maafisa wote wa polisi.

Kenya ina takriban maafisa laki moja wa polisi wanaofanya kazi katika jeshi hilo.

Bwana Mutyambai amesema walianza utaratibu wa kuwaondoa baadhi ya maafisa wa polisi walioathirika wakigusia umuhimu wa kuwa na polisi walio na akili timamu.

Hata hivyo amesema kuwaondoa maafisa hao katika kazi zao haikuwa rahisi kwa sababu ya mchakato unaohusika katika kuwaondoa.

Kumekuwa na wasiwasi zaidi katika miaka ya karibuni kuhusu akili za maafisa wa polisi na serikali ilianza kutatua suala hilo.

Bwana Mutyambai alisema kwa sasa polisi wana bodi ya kitaalamu ya afya inayojumuisha washauri na madaktari wa akili waliothibitishwa na Wizara ya Afya kutoa huduma ya afya ya akili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG