Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:29

Uchunguzi unaendelea jimbo la Virginia baada ya shambulizi la bunduki lililouwa watu sita


Shambulizi la duka la Walmart likiwa limezingirwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea.
Shambulizi la duka la Walmart likiwa limezingirwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Polisi katika jimbo la Virginia Marekani wanachunguza shambulizi la bunduki katika duka la Walmart  Jumanne jioni  ambalo limeua watu sita.

Mji wa Chesapeake ulisema mapema Jumatano kuwa polisi wamethibitisha idadi ya waliofariki, na mshambuliaji pia amefariki.

Mamlaka hazijasema alivyofariki mshambuliaji huyo au kutoa maelezo mengi kuhusu mazingira ya shambulizi hilo.

Mkutano na waandishi wa habari umepangwa kufanyika Jumatano asubuhi.

Walmart ilisema katika taarifa yake “imeshtushwa na tukio hili la maafa.”

“Tunawaombea wale walioathirika, jamii na wafanyakazi wetu. Tunashirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama, na tumejikita kuwasaidia wafanyakazi wetu,” kampuni hiyo ilisema.

Shambulizi katika duka la Walmart Virginia, Marekani.
Shambulizi katika duka la Walmart Virginia, Marekani.

Shambulizi limekuja siku chache baada ya shambulizi kwenye klabu ya usiku ya wapenzi wa jinsia moja LGBTQ huko Colorado Springs, Colorado, ambapo watu watano waliuawa na wengine 18 kujeruhiwa.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

XS
SM
MD
LG