Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 05:57
VOA Direct Packages

Uchaguzi wa Kenya 2022: ushindani mkali


Maafisa wa uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya, IEBC, wakihesabu kura.
Maafisa wa uchaguzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya, IEBC, wakihesabu kura.

Siku mbili baada uchaguzi mkuu Kenya, maafisa wa uchaguzi bado hawajatangaza nani anaongoza kinyang’anyiro hicho cha urais katika nchi yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki.

Wakati huo huo wananchi wamechanganyikiwa wakijaribu kufahamu majumuisho ya kura mbalimbali yanayochapishwa na vyombo vya habari katika ushindani mkali wa uchaguzi huo.

Mamlaka ya Uchaguzi nchini Kenya inaendelea kujumuisha matokeo kwa uangalifu, wakiwa makini wasifanye makosa yaliyosababisha Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi uliopita na kuamrisha urudiwe.

Vyombo vya habari vinajumuisha matokeo kutoka katika picha za fomu za uchaguzi ambazo tume ya uchaguzi imeziweka (kwenye tovuti) kutoka vituo vya kupiga kura zaidi ya 46,229 kwa kuwaajiri mamia ya watu kuja kuzitoa kutoka katika picha hizo na kuziingiza kwenye nyaraka za spreadsheets, kazi nzito ambayo inamaanisha majumuisho yao yako nyuma sana kulingana na kiwango cha takwimu zilizopo.

Majumuisho yao yanatoautiana kwa sababu matokeo kutoka katika vituo vya kupiga kura yaliwekwa katika tovuti kama yalivyokuwa yanawasili, na hivyo kila chombo cha habari kinahesabu sehemu ya fungu tofauti la kura hizo.

Kiongozi mkongwe wa upinzani na mfungwa wa zamani wa kisiasa Raila Odinga, miaka 77, anagombea kwa mara ya tano urais. Yuko karibu sana na Naibu Rais William Ruto, miaka 55 katika ushindani huu.

Hadi kufikia saa 1000 GMT Alhamisi, kampuni binafsi ya Nation ilikuwa imejumuisha matokeo kutoka robo tatu ya vituo vya kupiga kura na inamuweka Odinga akiongoza kwa asilimia 50.90yza kura na Ruto ana asilimia 48.42.

Wakati huo huo kampuni binafsi ya Citizen inaonyesha Ruto ana asilimia 49.48 ya kura na Odinga 49.12.

Baadhi ya wananchi wana wasiwasi kuwa tofauti za majumuisho yanayotolewa na vyombo vya habari zinaweza kuibua madai ya wizi wa kura, ambayo yalichochea machafuko katika chaguzi zilizopita. Wengi wanawasihi raia wenzao kusubiri matokeo rasmi.

“Uvumilivu umekosekana sana kutokana na ripoti za vyombo vya habari, kwa sababu wana tofautiana. Kutokana na uzoefu tulionao Kenya, ni lazima tuwe wenye kuvuta wastahmilivu na tusubiri,” alisema Ongao Okello, wakati akipitia magazeti yanayouzwa mtaani katika mji wa magharibi wa Eldoret.

Wagombea Willian Ruto na Raila Odinga
Wagombea Willian Ruto na Raila Odinga

Mgombea atakayeshinda lazima apate asilimia hamsini na nyongeza ya moja kupata ushindi, na angalau robo ya kura kutoka kaunti 24 kati ya 47 zilizoko Kenya. Kama hakuna mshindi, kutakuwa na duru ya pili ya upigaji kura bila ya wagombea hao wa urais kupata pointi yoyote.

Wakenya wengi, wamevunjika moyo kwa kubadilisha uungaji mkono wao wa viongozi wasomi na wamechoshwa na kupanda kwa bei na rushwa, hawakushiriki kupiga kura kabisa.

Tume imesema kiasi cha asilimia 65 ya waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza kuchagua wawakilishi, uchaguzi wa eneo na wa urais – ikiwa ni kushuka kwa idadi kubwa ukilinganisha na uchaguzi wa 2017 ambapo ushiriki wa wapiga kura ulikuwa kwa takriban asilimia 80.

Uchaguzi kwa kiasi kikubwa umekuwa wa amani hadi sasa; ghasia kubwa kawaida zinatokea wakati matokeo yanapotangazwa. Zaidi ya watu 1,200 waliuawa baada ya uchaguzi wa 2007, na zaidi ya 100 baada ya uchaguzi wa 2017.

Mwandishi wa vitabu na mchambuzi wa kisiasa Nanjala Nyabola alisema kutokuwepo ghasia isiwe ni kiwango cha kupima mafanikio.

“Watu wanaangalia kuwepo au kutokuwepo ghasia na kama Mkenya ni kipimo kinacho vunja moyo kutumika kama kipimo tukiambiwa kuwa tuwe na shauku kufikia hilo tu,” amesema mwanamama huyo. “Tunajaribu kufikia katika viwango vya juu.”

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG