Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:09

Kenya: Mashirika ya kiraia yaelezea wasiwasi juu ya habari za uongo kuhusu matokeo ya uchaguzi


Mfanyakazi wa tume ya uchaguzi akibeba masunduku ya kura kwenye kituo cha kukusanya na kujumlisha kura mjini Nairobi, Agosti 10, 2022. Picha ya AP
Mfanyakazi wa tume ya uchaguzi akibeba masunduku ya kura kwenye kituo cha kukusanya na kujumlisha kura mjini Nairobi, Agosti 10, 2022. Picha ya AP

Wakati Wakenya wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika kwa amani, shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International na mashirika kadhaa ya kiraia ya Kenya yameelezea wasiwasi juu ya “kuongezeka kwa habari za uongo au za kupotosha” zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wamesema Jumatano katika taarifa kwamba habari kadhaa zinazochapishwa na wagombea na wafuasi wao katika kambi pinzani za Odinga na Ruto “zilikuwa na lengo la kupotosha wapiga kura na umma juu ya mchakato wa uchaguzi na matokeo ya uchaguzi.

Matokeo ya awali yameonyesha ushindani mkali, lakini idadi ya waliopiga kura ilionekana iko chini kufuatia ongezeko la hasira dhidi ya viongozi wa kisiasa.

Naibu rais William Ruto na mwanasiasa mkongwe wa upinzani Raila Odinga aliyeungwa mkono na chama tawala, wameahidi kudumisha utilivu baada ya zoezi la kupiga kura Jumanne, lakini Wakenya wengi bado wanakumbuka ghasia zilizotokea katika uchaguzi wa miaka iliyopita.

Huku shinikizo likiongezeka kwa tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC) ambayo inatakiwa kutangaza matokeo ifikapo Agosti 16, maafisa wa tume hiyo walifanya kazi usiku kucha kuhesabu kura chini ya uangalizi wa waangalizi.

Mchakato mgumu wa kuhakiki na kujumlisha kura unatarajiwa kuchukua siku kadhaa, na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewataka Wakenya kuwa na subira, na kuepusha madai ya wizi ambayo yalikumba uchaguzi wa awali.

XS
SM
MD
LG