Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 07:25

Afisa wa IEBC amekamatwa kwa kupeana karatasi zaidi kwa wapiga kura anaofahamiana nao


Maafisa wa vituo vya kupiga kura wakijiandaa kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza Jumanne, Nairobi, Kenya.
Maafisa wa vituo vya kupiga kura wakijiandaa kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza Jumanne, Nairobi, Kenya.

Polisi wanamzuia afisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC kwa kuhusishwa na wizi wa kura.

wa kura.

Vyombo vya habari vya Kenya vinasema kwamba kamanda wa polisi wa kaunti ya Machakos Issa Mohammud amethibitisha kwamba afisa huyo wa IEBC amekamatwa baada ya kupatikana akipeana zaidi ya karatasi moja kwa baadhi ya wapiga kura anaofahamiana nao.

Tukio hilo limeripotiwa katika kituo cha kupigia kura cha Jyumbi, eneo bunge la Mavoko.

Mshukiwa, ambaye jina lake halijatajwa, atafikishwa mahakamani Jumatano Agosti 10 2022.

Polisi wamesema kwamba "afisa huyo wa IEBC alikuwa akipeana karatasi nane za kupigia kura badala ya sita kwa wapiga kura anaowajua.”

Mgombea wa kitu cha Gavana kaunti ya Machakos Nzioka Waita, wa Chama Cha Uzalendo amedai kwamba udanganyifu mkubwa umefanyika katika uchaguzi wa kaunti hiyo.

Amedai kwamba “kuna karatasi za kupigia kura zimepatikana nje ya kituo cha kupigia kura cha Muthwani, eneo bunge la Mavoko.”

Polisi wamesema kwamba wanachunguza kisa khicho. "Kulikuwa na tukio katika wadi ya Muthwani ambapo karatasi za kupigia kura zilipatikana nje ya kituo cha kupigia kura.”

XS
SM
MD
LG