Wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa iwapo utakuwa ni uchaguzi wa haki na huru utaipelekea nchi hiyo kurejea katika uchumi imara baada ya kuporomoka na kudidimia uchumi huo katika kipindi cha utawala wa Rais wa zamani Robert Mugabe.
Zoezi la uchaguzi mkuu linaloendelea maeneo mbalimbali Zimbabwe
Wananchi wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi mkuu Julai 30, 2018 wakati uchumi wa nchi hiyo umekabiliwa na changamoto nyingi.

1
Rais wa zamani wwa Zimbabwe, Robert Mugabe akipiga kura katika uchaguzi mkuu Harare, Zimbabwe, Julai 30, 2018

2
Kiongozi wa kambi kuu ya upinzani Zimbabwe Nelson Chamisa apiga kura katika kituo cha kupiga kura Zimbabwe, Jumatatu, Julai 30, 2018.

3
Wapiga kura nchini Zimbabwe wakisubiri kupiga kura katika uchaguzi mkuu mjini Harare, Julai, 30, 2018

4
Wafuasi wa mgombea urais wa chama cha upinzani Zimbabwe (MDC), Nelson Chamisa wakihudhuria mkutano wa mwisho wa kampeni za uchaguzi Harare, Zimbabwe, Julai 28, 2018.