Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:06

Uchaguzi mkuu Nigeria waahirishwa tena


Wapigaji kura walojipanga kwa mstari kusubiri kupiga kura katika kituo kimoja cha mjini Ibadan, Nigeria, Jumamosi Aprili 2, 2011, kabla ya kuarifiwa kwamba uchaguzi umeahirishwa.

Tume ya uchaguzi imetangaza kwamba uchaguzi wa bunge unaahisrishwa hadi Aprili 9, na uchaguzi wa rais na majimbo utaahirishwa pia.

Uchaguzi wa bunge wa Nigeria ulipangwa kufanyika tena Jumatatu tarehe Aprili baada ya kusitishwa kwa ghafla siku ya Jumamosi kama ilivyopangwa awali. Lakini maafisa wa uchaguzi walitangaza Jumapili kwamba uchaguzi mkuu kwa ujumla utacheleweshwa.

Maafisa wa uchaguzi wanalaumu matatizo ya kusambaza vifaa vya upigaji kura ndiyo yaliyosababisha kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu.

Kufuatana na ratiba mpya iliyotangazwa Jumapili uchaguzi wa bunge utafanyika Jumamosi ijayo, ukifuatiwa na uchaguzi wa rais Aprili 16 na ule wa magavana na majimbo Aprili 26.

Wakuu wa tume ya uchaguzi wanasema hivi sasa wameshapokea vifaa vyote vinavyohitajika na uchaguzi utafanyika bila ya matatizo. Maafisa hao wanakutana na wakuu wa vyama vya kisiasa na wagombea viti kujadili hali ya mambo.

Kuahirishwa kwa uchaguzi kulizusha hasira na kuvunjika moyo kwa watu wengi kote katika taifa hilo la Afrika lenye watu wengi kuliko nchi zote barani humo. Uchaguzi mkuu wa mwezi huu umechukuliwa kama mtihani kwa Nigeria kuweza kuanda uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika baada ya uchaguzi wa mwisho wa 2007 kuzusha ghasia na kugubikwa na wizi wa kura, na utayarishaji mbaya.

XS
SM
MD
LG