Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 11:19

Ghasia za zuka Nigeria baada ya Jonathan kutangazwa mshindi


Ghasia zilizozuka katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria baada ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais
Ghasia zilizozuka katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria baada ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais

Ghazia zimezuka kaskazini mwa Nigeria baada ya mkuu wa tume ya uchaguzi kutangaza kwamba Jonathan amemshinda Buhari katika uchaguzi wa rais.

Mara baada ya maafisa wa tume ya uchaguzi kumtangaza rais Goodluck Jonatha kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, ghasia zilizuka tena katika majimbo ya kaskazini yenye waislamu wengi nchini humo.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Attahiru Jega alitangaza kwamba Bw. Jonathan alipata kura milioni 22.5 katika uchaguzi wa Jumamosi ikiwa ni karibu mara mbili ya idadi ya kura alizopata mpinzani wake mkuu, kiongozi wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari, aliyepata kura milioni 12.2.

Rais Jonathan alipata kura za kutosha kuepusha duru ya pili ya uchaguzi kwa kupata asili mia 57 za kura zilizopigwa.

Habari hizo zilipotangazwa ghasia zilianza katika majimbo ya kaskazini. Chama cha Msalaba Mwekundu cha Nigeria kinakadiria kwamba zaidi ya watu 270 wamejeruhiwa na wengine elfu 15 wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia.

Rais Jonathan ametoa wito wa kusitishwa ghasia hizo mara moja. Lakini wafuasi wa upinzani wanasema kumekuwepo na wizi wa kura na wakatia moto nyumba, magari na kuwarushia mawe polisi katika kulalamika dhidi yamatokeo hayo.

Hakuna chama cha upinzani kilichotia saini hati ya matokeo rasmi ya mwisho na chama cha Bw Buhari kimefikisha mashtaka rasmi kupinga matokeo mahakamani.

XS
SM
MD
LG