Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:56

Ubalozi wa Marekani Kabul watahadharisha kuwepo uwezekano wa shambulizi


Wapiganaji wa Taliban Fateh, "kikosi maalum" wakilinda doria katika mtaa wa Kabul Agosti 29, 2021, wakati tishio la shambulizi la kujitoa muhanga likisikika siku chache kabla ya kumalizika operesheni ya kuondoa watu uwanja wa ndege wa Kabul. (Photo by Aamir QURESHI / AFP).
Wapiganaji wa Taliban Fateh, "kikosi maalum" wakilinda doria katika mtaa wa Kabul Agosti 29, 2021, wakati tishio la shambulizi la kujitoa muhanga likisikika siku chache kabla ya kumalizika operesheni ya kuondoa watu uwanja wa ndege wa Kabul. (Photo by Aamir QURESHI / AFP).

Saa chache baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kusema huenda shambulizi jingine linaweza kutokea kwenye wa ndege wa Kabul katika kipindi cha saa 24 hadi 36, Ubalozi wa Marekani mjini Kabul, ulielezea tishio maalum na la uhakika, umewataka raia wa Marekani kuondoka katika maeneo yaliyo karibu na uwanja wa ndege. 

Tahadhari ya usalama imewataka Wamarekani kuepuka kwenda uwanja wa ndege, na kusema wale walio karibu na uwanja huo, ikiwemo lango la Kusini (Airport Circle), Wizara ya mpya ya Mambo ya Ndani, na lango karibu na kituo cha petroli cha Panjshir upande wa kaskazini magharibi mwa uwanja wa ndege, ni vyemaz waondoke mara moja.

Biden alitahadharisha uwezekano mkubwa wa kuwepo mashambulizi katika taarifa yake ya Jumamosi, wakati Marekani na washirika wake wakikamilisha zoezi la kuwaondoa raia wake na Waafghanistan wanao wakimbia Taliban, siku mbili tu baada ya shambulizi la bomu la kujitoa muhanga katika eneo karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, ambapo sio chini ya watu 170 na wanajeshi wa Marekani 13 waliuawa.

Biden alisema aliwaelekeza makamanda wa Marekani kuwalinda wanajeshi wa Marekani walioko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamid Karzai wakati zoezi la kuondoa idadi kubwa ya watu kwa ndege likiwa linakaribia kumalizika na wanajeshi wa Marekani kuondolewa.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Takriban watu 2,000 walikuwa wameondolewa kutoka Kabul katika kipindi cha saa 12 hadi kufikia saa tisa mchana Jumamosi, kulingana na taarifa za White House. Zoezi hili lilihusisha kuondolewa watu 1,400 kwa ndege za kijeshi za Marekani na watu 600 kwa kutumia ndege saba za washirika 7.

White House pia imesema tangu Agosti 14, Marekani imewaondoa au kusaidia kuwaondoa kiasi cha watu 113,500. Tangu mwisho ni mwa mwezi Julai, Marekani imewahamisha kiasi cha watu 119,000.

Katika matukio mawili tofauti, shambulizi la anga lililofanywa na Marekani Ijumaa usiku dhidi ya kikundi cha washirika wa Islamic State cha Afghanistan – ikiwa ni kulipiza kisasi shambulizi walilofanya Alhamisi – limeua wanachama wawili muhimu wa kikundi hicho, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Jumamosi. Washirika hao, Islamic State Khorasan, au ISIS-K, walidai kuhusika na shambulizi lililofanywa uwanja wa ndege.

“Walengwa wawili wa ngazi ya juu wa ISIS waliuawa, na mmoja alijeruhiwa, na pia tuna taarifa za kutokuwepo vifo vya raia kabisa,” msemaji wa Pentagon John Kirby alisema katika mkutano wa waandishi.

“Shambulizi hili sio la mwisho,” Biden alisema. “Tutaendelea kumsaka yeyote aliyehusika katika shambulizi la kinyama na kuwawajibisha.”

Kirby hakujadili kwa kiasi gani uwezo wa ISIS utakuwa umedhoofika kufuatia shambulizi lililofanywa na Marekani, na badala yake akasema, “Wamempoteza mpangaji, na wamempoteza mwezeshaji, na mmoja wao amejeruhiwa. Na ilivyokuwa wawili hao hawawezi tena kutembea katika ardhi --- hilo ni jambo zuri.”

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ameripotiwa kulaani shambulizi la anga lililofanywa na Marekani, akisema ilikuwa ni “ni dhahiri ni katika ardhi ya Afghanistan,” kulingana na Reuters. Pia alirejea tena kusema Taliban wanatarajia kuchukua udhibiti kamili wa uwanja wa ndege wakati majeshi ya Marekani yatakapo kamilisha kuondoka nchini humo, kama ilivyopangwa ifikapo Jumanne.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Kirby alisema Jumamosi katika mkutano wa waandishi wa habari kuwa vitisho dhidi ya uwanja wa ndege “bado ni vya kweli, ambavyo vinaendelea, na sisi tunaendelea kuvifuatilia kwa uhalisia wake. Na, kama nilivyosema jana, tunachukua hatua zote muhimu kuhakikisha tunafuatilia mkondo huo wa vitisho na kufanya kila tunaloweza kuhakikisha tunajihami.

Vitisho hivyo vya usalama vimefanya zoezi la kuwaondoa Wamarekani na baadhi ya Waafghanistan kuwa gumu zaidi.

“Haionekani kama kuna juhudi zozote za kuwaondoa watu wenye visa maalum za uhamiaji, SIVs, wakati huu,” afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ameiambia VOA kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamid Karzai. Lakini wizara hiyo inaendelea kujaribu kuwaondoa raia wa Afghanistan waliokuwa wanafanya kazi ubalozini, raia wa Marekani na wakazi wa kudumu wa Marekani.

Zoezi la Marekani kuwaondoa Waafghanistan kutoka uwanja wa ndege limekaribia kumalizika, ambapo wafanyakazi wa kiraia 100 wa serikali ya Marekani wamepangiwa kuondoka kabla ya saa sita usiku, kulingana na afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje aliyezungumza na VOA Jumamosi kwa sharti asitajwe jina lake.

Sehemu nyingi katika uwanja wa ndege zilikuwa hazina watu, amesema afisa huyo, aliyeeleza hisia mseto kuhusu operesheni hiyo ya kuwaondoa watu.

XS
SM
MD
LG