Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 11:14

Serikali za magharibi zaonya kuwepo tishio la kigaidi Kabul

Watu wakipanda katika ndege tayari kuondolewa kutoka Afghanistan katika ndege ya kijeshi ya Jeshi la Anga la Marekani C-17 Globemaster III katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai. Agosti. 24, 2021. (Master Sgt. Donald R. Allen/U.S. Air Force via AP).

Serikali za Magharibi zilionya Alhamisi juu ya tishio la shambulizi la kigaidi katika uwanja wa ndege huko Kabul, Afghanistan.

Taarifa iliyotolewa inasema kwamba wale waliokusanyika katika eneo hilo wakitaka kuondoka nchini humo wanapaswa kuhamia eneo salama.

Kwa sababu ya vitisho vya usalama nje ya milango ya uwanja wa ndege wa Kabul, tunashauri raia wa Marekani waepuke kusafiri kwenda uwanja wa ndege.

Pia wametakiwa kuepuka kutumia milango ya uwanja wa ndege wakati huu isipokuwa tu wakipokea maagizo binafsi kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Marekani kufanya hivyo, Ubalozi wa Marekani mjini Kabul ulisema katika taarifa.

Waziri anayehusika na Jeshi la Uingereza James Heappey aliiambia BBC, kwamba kuna ripoti za kuaminika sana kuhusu shambulizi la kigaidi.

XS
SM
MD
LG