Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:24

Uamuzi wa ECOWAS kuhusu sheria za uandishi wa habari wapongezwa


Muonekano wa jengo la bunge huko Abuja Nigeria. Picha na REUTERS/Afolabi Sotunde
Muonekano wa jengo la bunge huko Abuja Nigeria. Picha na REUTERS/Afolabi Sotunde

Watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari nchini Nigeria wanapongeza uamuzi wa karibuni wa mahakama ya Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS ulioitaka mamlaka ya Nigeria kupitia upya vifungu vya Sheria ya Vyombo vya Habari nchini humo.

Mahakama ilisema vifungu vya sheria vinawabagua waadnishi wa habari wa mtandaoni na wasio na taaluma. Uamuzi huo ulikuja baada ya waandishi wa habari wawili wa Nigeria kufungua kesi dhidi ya mamlaka mwaka 2021.

Waandishi wa habari wa Nigeria Isaac Olamikan na Edoghogho Ugberease waliwasilisha kesi yao katika mahakama ya ECOWAS miaka miwili iliyopita baada ya waandishi hao kukamatwa na maafisa wa usalama katika matukio tofauti wakati walipokuwa wakikusanya habari.

Olamikan alituhumiwa kuandika habari akiwa na kibali cha uandishi wa habari ambacho kimekwisha muda wake.

Ugberease – ni mwanahabari ambaye mara nyingi aliandika matukio katika jamii yake ya eneo la kusini mwa Nigeria katika jimbo la Edo - aliambiwa na mamlaka kuwa hakuwa na vigezo vinavyotakiwa kuandika habari au kufanya uchunguzi.

Hata hivyo, jopo la watu watatu wa mahakama ya ECOWAS lilitoa uamuzi kwamba vifungu vitatu vya Sheria ya Baraza la Habari la Nigeria vimeweka vikwazo vya umri na sifa za elimu kwa waandishi wa habari na hivyo kuwabagua waandishi wa kiraia wa habari za mtandaoni

Mahakama ilisema kuwa maendeleo ya teknolojia yanamaanisha mabadiliko ya vyombo vya habari, lakini sheria ya Nigeria imeshindwa kukubaliana na mabadiliko hayo.

Ahaziah Abubakar, mkurugenzi wa zamani wa habari katika Voice of Nigeria, alisema hukumu ya ECOWAS imekuja katika muda muafaka zaidi ya huu.

Forum

XS
SM
MD
LG