Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 05:29

Tume ya uchaguzi Zanzibar yamtangaza Hussein Mwinyi mshindi wa urais 


Rais Hussein Mwinyi

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi, CCM, Hussein Mwinyi ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar.

Ushindi huu umetangazwa wakati Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye ni mgombea wa urais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Seif Sharif Hamad akiwa amekamatwa Alhamisi. Hii ni mara ya pili kukamatwa.

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inasema kuwa Mwinyi ameshinda kwa asilimia 76. 27% wakati mpinzani wake wa Chama cha ACT- Wazalendo Maalim Seif akiwa ni mshindi wa pili kwa kura asilimia 19.87%.

"Nimepokea ushindi kwa mikono miwili, nashukuru kuwa wananchi walio wengi wamenichagua mimi na chama changu cha Mapinduzi kwa miaka mitano ijayo,” amesema Rais Mwinyi mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.

"Nawashukuru kwa uvumilivu na ustahamilivu mkubwa. Nawashukuru zaidi kwa kunipigia kura za kutosha kuwa rasi wa Zanzibar. Nitalipa imani hii kwa utumishi uliotukuka," Mwinyi alisema.

Mwinyi ameeleza pia kuwa Zanzibar mpya itajengwa na Wazanzibari wote bila kujali itikadi, Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofuati hizo.

"Mimi Hussein Mwinyi si bora kuliko CCM, ushindi huu ni wa Wazanzibari wote ,uchaguzi sasa umekwisha turudi kujenga Zanzibar mpya.”

Aidha amesisitiza wafuasi wa CCM, washeherekee kwa ustaarabu bila ya kukwaza wengine kwa kuwa ushindi wasingepata pasipo kuwa na ushindani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG