Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 23:41

Tsunami Indonesia : Watu 222 wapoteza maisha, 843 wajeruhiwa


Athari za Tsunami iliyotokea nchini Indonesia Jumamosi.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na janga la tsunami lililotokea Jumamosi usiku katika visiwa vya Java na Sumatra nchini Indonesia imefika 222 na kuhofiwa itaongezeka huku wengine 843 wamejeruhiwa na karibu 28 hawajulikani walipo.

Idara ya hali ya hewa na jiolojia, BMKG, imeripoti kuwa Tsunami imetokea karibu saa tatu na nusu usiku, nusu saa baada ya kulipuka kwa mlima wa volcano wa Anak Krakatoa.

Idara inaeleza kwamba huwenda tsunami imesababishwa na mchanganiko wa mambo ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa ardhi chini ya bahari baada ya mlipuko wa volcano pamoja na mawimbi makubwa yaliyo sababishwa na mwezi mpevu.

Msemaji wa idara ya kukabiliana na majanga ya kitaifa, BNBP, ameeleza kwamba mamia ya nyumba, hoteli 9 na zaidi ya boti 350 zimeharibika pamoja na mamia ya magari na vyombo vingine vya usafiri.

Rais Joko Widodo wa Indonesia ameamrisha idara zote za serikali kusaidia kwa haraka maeneo yaliyokumbwa na maafa.

Tsunami hiyo imetokea karibu na mahala ambako tetemeko kubwa la Disemba 26, 2004 pamoja na tsunami iliyofuata ilisababisha vifo vya watu 226, 000 katika nchi 13 pamoja na Zaidi ya 120,000 huko Indonesia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG