Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 09:40

Tshisekedi ataka ushirikiano wa dhati na WHO kuchunguza kashfa ya ngono


Rais Félix Tshisekedi (Photo by EDUARDO MUNOZ / POOL / AFP)

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi anasema anataka ushirikiano wa kweli na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuchunguza tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono.

Amesema tuhuma hizo zinawakabili watumishi wa shirika hilo waliopelekwa kupambana na mlipuko wa Ebola nchini DRC.

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya amekiambia kituo cha televisheni cha taifa Jumamosi kwamba Rais Tshisekedi ametoa wito huo wa kutaka ushirikiano wa dhati kati ya taasisi na vyombo vya serikali na mashirika ya kimataifa yaliyopewa jukumu la kufuatilia kashfa hiyo.

Maeneo yaliyokumbwa na mlipuko wa Ebola DRC Feb. 22, 2021
Maeneo yaliyokumbwa na mlipuko wa Ebola DRC Feb. 22, 2021

Wito wa kiongozi wa DRC umetolewa kufuatia ripoti kali iliyotolewa siku ya Jumanne ikibaini kasoro kubwa katika mfumo wa kazi na uzembe wa watu miongoni mwa wafanyakazi wa WHO baada ya wanawake kadhaa kuwaambia wapelelezi kwamba waliambiwa wafanye vitendo vya ngono ili waweze kupewa kazi au walikuwa waathirika wa ubakaji.

Ripoti imezingatia tuhuma dhidi ya wafanyakazi wa Congo na wa kimataifa waliofanya kazi nchini humo kupambana na mlipuko wa Ebola kuanzia 2018 hadi 2020.

“Rais Tshisekedi ameeleza kusikitishwa kwake na kulaani vitendo hivyo viovu na wakati huo huo kusifu ushujaa wa WHO kwa kulaani hadharani uhalifu uliotendwa na wafanyakazi wake” alisema msemaji wa serikali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG