Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:18

Timu ya Trump yagawanyika katika uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Nje


Mgombea urais wa zamani Mitt Romney na Meya wa zamani wa New York City Rudolph Giuliani watajwa katika uteuzi huo
Mgombea urais wa zamani Mitt Romney na Meya wa zamani wa New York City Rudolph Giuliani watajwa katika uteuzi huo

Mgawanyiko katika timu ya mpito ya Rais-mteule Donald Trump kuhusu nani ateuliwe kuwa waziri wa mambo ya nje umeanza kutoka hadharani, na kusababisha nafasi hiyo kubaki wazi mpaka tofauti ndani ya timu hiyo zipatiwe ufumbuzi.

Makundi yanayopingana katika timu hiyo ya mpito yamegawanyika baina ya mgombea urais Mrepublican mwaka 2012 Mitt Romney na meya wa zamani wa jiji la New York Rudolph Giuliani.

Katika ujumbe wa Twitter Alhamisi, mshauri wa Trump, Kellyanne Conway alieleza hisia za upande unaompinga Romney. Conway alisema amepata "rundo" la maoni yenye wasiwasi ambayo yanahoji utiifu wa Romney ambaye alimshambulia sana Trump wakati wa kampeni za urais.

Wale wanaompinga Giuliani kama waziri wa mambo ya nje wanadai kuwa uhusiano wake mkubwa na makampuni ya nje huenda ukasababisha mvutano mkubwa katika vikao vya kumthibitisha katika baraza la seneti. Wanahoji pia endapo mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 ana nguvu za kuweza kuwa anasafiri sana nje ya nchi kama kazi hiyo inavyohitaji.

Rais huyo mteule, ambaye amejizolea sasa sifa ya kugeuza misimamo yake, amewasifu wote Romney na Giuliani. Trump inasemekana aliwaambia wasaidizi wake kwamba Romney "anafanana" na nafasi hiyo lakini pia amekuwa akimsifu Giuliani pia.

Wengine ambao wanasemekana kufikiriwa katika nafasi hiyo ni pamoja jenerali mstaafu na mkurugenzi wa zamani wa CIA David Petraeus na Seneta Bob Corker wa Tennessee.

XS
SM
MD
LG