Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 11:29

Trump amemteuwa bilionea Ross kuwa waziri wa biashara


Rais mteule wa Marekani Donald Trump(L) akiwa na Wilbur Ross. Nov. 20, 2016.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump(L) akiwa na Wilbur Ross. Nov. 20, 2016.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kumteuwa mwekezaji bilionea, Wilbur Ross kama waziri wa biashara.

Ross mwenye umri wa miaka 78 ni mwenyekiti wa kampuni binafsi ya W.L.Ross &Co ambayo inafahamika kwa kununua makampuni yaliyoshindwa kujiendeleza kibiashara. Rais Mteule Donald Trump yupo katika kipindi cha kuunda baraza lake la mawaziri ambapo Jumatano alishamteuwa gavana wa jimbo la South Carolina, Nikki Haley kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa. Haley gavana wa mihula miwili katika jimbo hilo ni mtoto wa kike wa wazazi wahamiaji kutoka India.

Pia rais huyo mteule alimteuwa Betsy Devos kuwa waziri wa elimu. Haley na Devos ndio wanawake pekee kwa sasa katika orodha ya baraza la mawaziri lililojaa wanaume wazungu.

XS
SM
MD
LG