Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:05

Trump athibitisha alirejesha pesa zilizolipwa na wakili wake


Rais Donald Trump (kushoto), Stormy Daniels
Rais Donald Trump (kushoto), Stormy Daniels

Wakili mpya wa Rais Donald Trump, meya wa zamani wa mji wa New York, Marekani Rudy Giuliani amesema kwamba Trump alimrejeshea wakili wake binafsi kiasi cha Dola za Marekani 130,000 alizomlipa mcheza filamu za ngono Stormy Daniels.

Stormy Daniels alipewa pesa hizo ili kumnyamazisha kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016 ili asizungumzie uhusiano wake wa ngono anaodai uliokuwepo kati yake na Trump

Giuliani aliyejiunga hivi karibuni na timu ya mawakili wa Trump alitoa maelezo hayo wakati wa mahojiano na kipindi cha runinga cha kituo cha televisheni ya Fox news ambayo yanatofautiana na taarifa aliotoa Trump kuhusu pesa hizo ambazo zimezua kashfa kubwa.

Mwezi mmoja uliopita, Trump alisema kwamba hana taarifa kuhusu malipo yanayodaiwa kutolewa na Stormy Daniels ikiwa sehemu ya mkataba ambao mcheza filamu huyo alisaini akikubali hatatoa taarifa kuhusu uhusiano wao kabla ya uchaguzi mkuu. Trump amekanusha kuwa na uhusiano wowote na Daniels.

XS
SM
MD
LG