Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 11:52

Trump atangaza tarehe ya kukutana na Kim


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Alhamisi atafanya mazungumzo na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, ifikapo tarehe Juni 12, huko Singapore.

Trump ameandika kwenye ujumbe wake wa twitter “ kwamba wote wawili watajaribu kuufanya mkutano huo kuwa tukio maalum kwa ajili ya amani ya dunia.”

Trump ameeleza hayo baada ya kuwapokea raia watatu wamarekani waliowasili baada ya kuzuiliwa kwa muda huko Korea ya Kaskazini.

Trump amesisitiza kwamba lengo kuu la mkutano wake na Kim UN ni kuitaka Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa silaha za nyuklia.

Rais Trump aliwapokea Wamarekani hao watatu akifuatana na Makamu Rais Mike Pence na wake zao. Waliwasili katika kituo cha kijeshi cha Joint Base Andrews, Jiimbo la Maryland, Marekani Mei 10, 2018.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG