Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 23:39

Pompeo afanikisha kuachiwa raia watatu wa Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Rais wa Marekani Donald Trump amesema raia watatu wa Marekani waliokuwa wanashikiliwa Korea Kaskazini wameachiliwa huru na wako njiani kurejea Marekani.

Raia hao wamefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo.

Trump ameandika katika akaunti yake ya Twitter kwamba raia hao wa Marekani wenye asili ya Korea Kaskazini wako katika hali nzuri na afya njema na amesema anajiandaa kuwakaribisha (kuwapokea) watakapo wasili Marekani.

Kuachiliwa kwa watu hao ni matokeo ya ziara ya Waziri Pompeo alioifanya huko Korea Kaskazini na kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, ikiwa ni katika mchakato wa kuandaa mkutano utakao wakutanisha Rais Trump na Kim Un ambao unalengo la kumaliza mvutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG