Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:59

Trump azishutumu idara za kipelelezi na vyombo vya habari


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump ameanzisha mashambulizi mapya Jumatano dhidi ya vyombo vya habari vilivyokuwa vinazungumzia mahusiano yake na Russia, akiilaumu Jumuiya ya kijasusi kwa kile alichokiita kuvujisha taarifa nyeti “kinyume cha sheria” kwa vyombo vya habari.

“Zile taarifa za siri ambazo zinatolewa kinyume cha sheria na 'majasusi' kama vile wanagawa peremende ni aibu kubwa. Huu si uzalendo!” Trump amesema.

Katika mlolongo wa maoni yake kwenye Twitter, Trump ameelezea kuwa habari zenye maelezo yanayo mhusisha yeye, wasaidizi wake wa kampeni na mshauri wa usalama wa taifa aliyejiuzulu, Michael Flynn na maafisa wa Russia zilikusudia kukanusha ushindi wake katika uchaguzi wa Novemba.

Trump, ambaye ameshika madaraka kwa kipindi kisichozidi miezi miwili, amesema katika ujumbe wake wa Twitter, “Suala la kunihusisha na Russia ni upuuzi mtupu, na ni jaribio tu la kufunika makosa mengi ya Hillary Clinton katika kushindwa kwake kwenye kampeni.”

Amesema “vyombo vya habari feki vimechanganyikiwa na nadharia zao ni zenye njama na chuki zisizo na msingi.”

Ameongeza kuwa vituo viwili vya habari feki, MSNBC na CNN, “havistahili kuangaliwa”, wakati akielezea kipindi kinachoitwa “Fox & Friends” kinacho onekana katika kituo cha televisheni cha “Fox News”,kwamba ni “bora.”

Wakati huo huo rais amedai kuwa “taarifa zimekuwa zikitolewa kinyume cha sheria kwa magazeti yasiyoaminika” New York Times na Washington Post na Jumuiya ya Kijasusi, Idara ya Upelelezi na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, “kama inavyotokea Russia.”

Gazeti la The Post wiki iliyopita lilikuwa la kwanza kuandika kwa kina juu ya mazungumzo kati ya Flynn na balozi wa Russia huko Washington kabla Trump hajakabidhiwa ofisi, wakati jarida la Times katika toleo lake la Jumatano limesema wasaidizi wa Trump na washirika wake walikuwa wana mawasiliano ya mara kwa mara na maafisa wa ngazi ya juu wa Russia wakati wa kampeni 2016.

Rais pia alimshambulia mtangulizi wake rais mstaafu Barack Obama, akisema, “Russia waliichukua Crimea iliyokuwa chini ya utawala wa serikali ya Ukraine wakati wa uongozi wa Obama. Je Obama pia alikuwa mdhaifu kwa Russia?"

Obama aliionya Moscow kwa kitendo chake cha kufanya uamuzi binafsi juu ya kuivamia peninsula ya Crimea. Uongozi wa Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya, wakaiwekea vikwazo Russia. Lakini nchi za magharibi hazikuingilia kati kijeshi na Crimea imebakia kuwa chini himaya ya Russia.

Russia imetupilia mbali ripoti za jarida la Times kwamba timu ya kampeni ya Trump na washirika wake walikuwa na mawasiliano na maafisa wa ngazi za juu wa kijasusi wa Russia kabla ya uchaguzi wa Marekani Novemba mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG