Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:28

Trump aitetea ICE kuwa inafanya kazi nzuri


Rais Donald Trump wa Marekani
Rais Donald Trump wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumapili ali-itetea idara iliyohusika kudhibiti wahamiaji nchini Marekani-ICE dhidi ya wito kutoka kwa baadhi ya wapinzani wa Democrat kwamba ifutwe

Rais Trump aliandika kwenye Twitter kwamba wa-Liberali wa mrengo wa kushoto pia wanajulikana kama wa-Democrat wanataka kufutwa kwa ICE ambayo inafanya kazi nzuri na wanataka mipaka kuachwa wazi. Uhalifu utakuwa mwingi na hautaweza kudhibitiwa.

Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Fox News cha Marekani, Rais Trump alisema kutoka mtazamo wake wa kisiasa kwamba analipenda suala hilo linalohusu uhamiaji. Aliendelea kusema kwamba kama wademokrati wanaendelea na wito wao wa kufuta idara hiyo kwa matamshi yake “ninafikiri hawataweza kushinda uchaguzi mwingine”.

Waandamanaji wanaopinga sera za Trump kwa wahamiaji
Waandamanaji wanaopinga sera za Trump kwa wahamiaji

Maelfu ya waandamanaji waliandamana Jumamosi nchi nzima ya Marekani dhidi ya sera ya utawala wa Trump ya kutostahmili wahamiaji hususan suala la hivi karibuni la watoto kutenganishwa na familia zao kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

XS
SM
MD
LG