Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 07:38

Mapambano yazuka kati ya polisi, waandamanaji Iran


Maandamano nchini Iran

Vyombo vya habari vya taifa nchini Iran vimeripoti kuwa kumekuwa na mapambano jioni Jumapili kati ya polisi na waandamanaji wanao athiriwa na ukosefu wa maji na uchafuzi wa mazingira kusini magharibi mwa Iran.

Shirika la habari la Iran IRNA limesema kuwa waandamanaji hao katika mji wa Abadan waliwatupia mawe na makorokoro mengine polisi, na kuwa maafisa wa polisi waliweza kudhibiti hali hiyo.

Mapema usiku, kulikuwa na mapambano kama hayo yaliyo fanywa na waandamanaji ambao wana athiriwa na uhaba wa maji katika mji wa karibu wa Khorramshahr ambapo watu kadhaa walikuwa wamejurihwa.

Picha za video zilikuwa katika mitandao zikionyesha waandamanaji wakitupa mawe na kukabiliana na vyombo vya usalama, wakati televisheni ya taifa ilikuwa inaonyesha picha za majengo ambayo yalikuwa yamevunjwa vioo. Mirindimo ya risasi ilikuwa ikisikika katika baadhi ya video hizo. Polisi walirusha mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji.

Waziri wa Mambo ya Ndani Abdolreza Rahmani Fazli amesema hakuna mtu aliye uwawa katika mapambano hayo huko Khorrmshahr. Naibu wake Hossein Zolfaghari amesema watu 11 walijeruhiwa , wakiwemo maafisa wa polisi 10 na raia mmoja.

Sehemu kubwa ya Iran inakabiliwa na ukame, ambapo wachambuzi wanasema serikali imefanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya usimamizi mbaya.

Nchi hiyo imeshuhudia maandamano kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, yakiwemo yale maandamano yaliyo fanyika wiki iliyopita Tehran, katikati ya sakata la kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iran na kuongezeka mfumuko wa bei.

Hali hiyo ya uchumi inakabiliwa na ongezeko la shinikizo la vikwazo tangu Rais wa Marekani Donald Trump kufanya maamuzi mwezi Mei kujiondoa kutoka katika makubaliano ya kimataifa ya kusitisha programu ya nyuklia ya Iran kwa kubadilishana nao na kupunguzwa kwa vikwazo vya kiuchumi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG