Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 02:48

Trump asikitishwa na uamuzi wa mahakama


Rais Donald Trump akiwa katika mkutano na baraza lake la mawaziri ikulu ya White House, Washington, Januari 10, 2018.

Ikulu ya White House imesema Jumatano imesikitishwa na kitendo cha Jaji wa serikali kuu kumuamrisha Rais Donald Trump kuendeleza programu inayowalinda maelfu ya wahamiaji kutoondolewa nchini (DACA) ambao waliingia kinyume cha sheria wakati walipokuwa watoto.

Msemaji wa Ikulu ya White House Sarah Sanders amesema “ jambo lenye uzito kama huu lazima lipitie katika mchakato wa kawaida wa utungaji sheria.”

Amesema Trump “ anakubaliana bila mashaka na utawala wa sheria, na atafanya kazi na vyama vyote viwili kufikia suluhu ya kudumu ambayo itasahihisha hatua ambazo ni kinyume cha katiba” ambazo zilichuliwa na mtangulizi wake Trump, mstaafu Rais Barack Obama, katika kuandaa programu ya kuwalinda wahamiaji vijana wanaofikia 800,000 ili wasiondolewe nchini.

Pia Trump ameshambulia uamuzi ambao unahusu hatua ya progamu ya kuchelewesha kuchukuliwa hatua kwa watoto walioingia nchini (DACA), akisema “inamuonyesha kila mtu vipi Mfumo wa Mahakama ulivyokuwa hauna uadilifu na umefeli ni “pale wapinzani wa maamuzi yake aghlabu wanafungua mashtaka dhidi yao katika mahakama zilizoko magharibi ya Marekani “ na mara nyingi wanashinda kabla uamuzi huo haujatenguliwa na Mahakama za Juu.

Hasira za Trump zilikuwa zinaelekezwa kwa Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani William Alsup huko California, ambaye alitoa uamuzi uliowapa ushindi kikundi cha watu binafsi na taasisi, kikiwemo Chuo Kikuu cha California, ambaye aliishtaki serikali yake ambayo ilikuwa inataka kuzuia kusitishwa kwa programu ya DACA.

Hatimaye Trump aliliambia Baraza lake la Mawaziri katika mkutano uliofanyika White House, “Tunataka kuona hatua zinachukuliwa katika suala hili la DACA, kwani imekuwa ikizungumziwa kwa miaka mingi sasa na watoto hawa wamekwisha kuwa watu wazima, katika masuala mengi.

Trump ameongeza kuwa “ Juu ya yote hayo, muswada wowote tunaoupitisha lazima uangalie jinsi ya kuboresha ajira, malipo na usalama wa wananchi wa Marekani. Watu waliotuchagua, sote sisi, watu hao waliotuchagua, lazima tuwasimamie vizuri, wote hao kwa ujumla.”

Mnamo mwezi Septemba, Trump alisitisha programu ya DACA, lakini alilipa Bunge la Congress mpaka Machi 5 kutathmini suala hilo, ambapo alijadiliana kwa kina na wabunge wa Marekani Jumanne katika mkutano wa Ikulu ya White House ambao nadra huonyeshwa kwenye luniga.

Amri hiyo ya mahakama inayoiendeleza programu ya DACA inahusu taifa zima, na mahakama ikisema kuwa suala hilo linamgusa kila raia wa kila jimbo la Marekani na nchi yote.

Amri ya mahakama ya Jumanne inaainisha kuwa vipengele vyote vya programu ya DACA zitaendelea kufuatwa kwa mtu yoyote aliyekuwa tayari ameingizwa katika programu hiyo kabla ya hatua ya Trump kutangazwa na kuwa watu wote hawa wanaruhusiwa kujiandikisha upya.

Lakini serikali haipaswi kushughulikia maombi mapya kwa watu wanaojaribu kujiandikisha katika programu ya DACA kwa mara ya kwanza, na wana hiari ya kumsafirisha mtu yoyote ambaye ni hatarishi kwa usalama wa taifa au ni tishio kwa usalama wa umma.

Amri hiyo ya mahakama imetolewa masaa kadhaa baada ya Trump kuwaambia wabunge kuwa atasaini sheria yoyote ya DACA ambayo watakubaliana nayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG