Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:39

Toni Morrison atakumbukwa kwa uandishi wa fasihi, historia ya Marekani


Marehemu Toni Morrison
Marehemu Toni Morrison

Toni Morrison ambaye ni mwandishi, mwanazuoni na mhariri wa kizazi chake aliaga dunia wiki hii akiwa na umri wa miaka 88.

Morrison ambaye ni mshindi wa tuzo ya Laureate, athari yake katika fasihi ya Marekani na barua zake hazina mfano kwa wafuasi wake.

Katika shule mbalimbali nchini kote Marekani, vizazi vingi vya wanafunzi hao waliweza kufahamu utumwa, ubaguzi na historia ya Marekani na bila ya vitabu vyake kama vile “Beloved,” “Sula,” na “The Bluest Eye” – na katika namna ambayo, miongo baada ya miongo, Wamarekani wengi wamekuja kugundua hatuwezi kujitambua bila ya historia.

Kutoka miaka ya 1960 hadi mwaka 1980 kama mhariri katika Kampuni ya Random House, alikuwa akiwafundisha kikundi cha waandishi mchanganyiko na kuweza kaunzisha zama mpya za kupaza sauti mbalimbali zenye umahiri na nia yao binafsi ya kujiendeleza pamoja na kuwepo vipingamizi.

Katika mahojiano na mshairi Sonia Sanchez, alieleza kuwa kitabu chake cha kwanza alicho hariri wakati huo ni cha Boris Bittker, kinachoitwa “The Case for Black Reparations,” na kusema “sehemu ya shughuli za kuhariri ni kuwaambia watu wanyamaze.”

Mnamo mwaka 1987, alichapisha kitabu “Beloved,” na mwaka 1993, alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kimarekani kushinda tuzo ya Nobel (baada ya kuchapisha kitabu chake cha kwanza,” “The Bluest Eye,” akiwa na umri wa miaka 40).

Mwaka 1990, alibuni mawazo yenye msimamo mkali kwa niaba ya wanafunzi wake katika Chuo Kikuu cha Princeton kwa kubuni na kuendeleza Warsha aliyoianzisha Princeton, ambayo hivi leo imewaleta waandishi mbalimbali katika chuo hicho ili kushirikiana na wanafunzi wa chuo hicho kwa karne nyingi.

I

XS
SM
MD
LG