Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:54

Mjumbe wa Marekani akamilisha ziara Burundi.


Wasuluhishi wa mzozo wa Burundi. wakiwa kwenye mazungumzo Bujumbura.
Wasuluhishi wa mzozo wa Burundi. wakiwa kwenye mazungumzo Bujumbura.

Mjumbe maluum wa rais wa Marekani katika kanda ya maziwa makuu amemaliza ziara yake ya siku mbili jijini Bujumbura Alhamisi .

Katika ziara hiyo Tom Perriello alikutana kwa mazungumzo na viongozi kadhaa wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, makamu wake wa kwanza Gaston Sindimwo na spika wa Bunge la taifa ambaye pia ndiye mkuu wa chama tawala nchini humo Pascal Nyabenda.

Ziara hiyo ilikuwa ni kwa lengo la kushinikiza serikali kukubali kukaa kwenye meza moja na wapinzani wake ili kumaliza tofauti zao kwa amani. Hii ni baada ya mazungumzo chini ya usimamizi wa rais wa Uganda Yoweri Museveni yaliyozinduliwa jijini Entebbe Uganda mwishoni mwa mwaka jana kukwama.

Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa tangu Aprili mwaka jana pale rais wa nchi hiyo alipotangazwa na chama chake kuwa atagombea urais kwa muhula wa tatu.

XS
SM
MD
LG