Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 17:34

Tinubu adai baadhi ya wanasiasa wanachochea maandamano Nigeria


Picha ya maandamano Nigeria.
Picha ya maandamano Nigeria.

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, Jumapili ameomba kusitishwa kwa maandamano dhidi ya hali ngumu ya kiuchumi, akisema kuwa yamegeuka kuwa ghasia, huku akilaumu baadhi ya watu wenye ajenda za kisiasa kwa kuchochea hali hiyo.

Maandamano hayo yalioanza Alhamisi yanadaiwa kusababisha wizi na uharibifu wa mali, huku maafisa wa usalama wakidaiwa kutumia nguvu kupita kiasi. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, shirika la Kimataifa la Amnesty International, limeripoti vifo vya watu 9, kufutia makabiliano na polisi, wakati wengine wanne wakiuwawa kwenye shambulizi la bomu.

Hata hivyo idara ya polisi ya Nigeria imekanusha madai hayo. “ Nimewasikiliza na kuwaelewa vyema,” Tinubu amesema. “Naelewa masaibu yenu, yaliopelekea maandamano haya, na ningependa kuwahakikishia kuwa serikali yetu imewasikia na ipo tayari kuyashugulikia,” ameongeza kusema.

Hata hivyo amesema kuwa vikosi vya usalama vitashugulikia watu wachache wenye ajenda za kisiasa zinazoweza kusambaratisha nchi. Ushindi wa Tinubu wa asilimia 37 kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana ulipingwa na upinzani, ukiwa ushindi mdogo zaidi wa rais katika historia ya Nigeria.

Uchaguzi huo pia unasemekana kuvutia wapiga kura wachache zaidi tangu 1999, pale taifa hilo lilipokumbatia utawala wa kidemokrasia.

Forum

XS
SM
MD
LG