Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 22:08

Watu 19 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa kwa bomu nchini Nigeria


Ramani ya Nigeria ikionyesha jimbo la Borno ambako kumetokea mlipuko wa bomu.
Ramani ya Nigeria ikionyesha jimbo la Borno ambako kumetokea mlipuko wa bomu.

Maafisa wa usalama na serikali wanasema bomu lilitokea takriban kilomita 50 kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno huko Maiduguri

Maafisa katika jimbo la Borno nchini Nigeria wanasema watu 19 waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa wakati bomu lilipolipuka katika nyumba maarufu ya chai Jumatano jioni, ikiwa ni shambulio la pili kubwa katika wiki za hivi karibuni.

Maafisa wa usalama na serikali wanasema bomu hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Kawuri, takriban kilomita 50 kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno, huko Maiduguri, ambako maafisa wanasema waliojeruhiwa walipelekwa hospitali kwa matibabu.

Maafisa wanasema bomu hilo lilitegwa na halikuwa shambulio la kujitoa muhanga. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini kundi la jihadi la Boko Haram na wapinzani wao, Islamic State West Africa Province, wote wanafanya harakati zilizo hai katika jimbo la Borno.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo, mamlaka za Nigeria zinaweza kuweka vizuizi vya kutembea, ukaguzi wa magari, au amri ya kutotoka nje kwa muda mfupi ili kukabiliana na shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG