Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 03:53

Tillerson aitaka Russia kuacha kumsaidia Assad


Rex Tillerson

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema anategemea Russia itaacha kumsaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad baada ya shambulizi la kutumia silaha za kemikali wiki iliopita.

“Niwazi kwetu sote kuwa utawala wa mabavu wa familia ya Assad unakaribia kufikia mwisho, “Tillerson amesema wakati akiwa Itali ambako alikuwa akihudhuria mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa G-7.

Syria ndio imekuwa ikilengwa na mazungumzo hayo ambayo yanafanyika kabla ya ziara ya Tillerson huko Moscow ambako anatarajiwa kukutana na maafisa wa Russia.

Kandoni mwa mkutano huo wa Italy, Tillerson amefanya mikutano na mawaziri wenzie kutoka Jordan, Qatar, Saudi Arabia, Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu

‘Mchezo sasa umebadilika’

Baada ya mkutano wake na Tillerson Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amesema kwamba baada ya Marekani kushambulia kwa makombora kituo cha kijeshi cha anga cha Syria, “ Mchezo sasa umebadilika.”

Johnson amesema kuwa washirika wote watakuwa wanajadili kuongeza vikwazo dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Syria, na pia wahusika katika jeshi la Russia ambao wamekuwa wakiratibu juhudi za Syria na ni kama alivyosema Johnson, “wameharibiwa na udhalimu wa tabia ya utawala wa Assad.”

Baadae Jumatatu, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May aliongea kwa simu na Rais Donald Trump. Ofisi yake May imesema viongozi hao wawili wamekubali kuwa hivi sasa kuna “fursa imejitokeza” kuishawashi Russia kwamba kuendelea kuwa upande wa Syria sio katika maslahi ya nchi hiyo.

Tamko la ikulu ya White House kuhusu mazungumzo hayo, na yale kati ya Trump na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, kwamba wote watatu wanakubaliana juu ya umuhimu wa kumwajibisha Rais wa Syria Bashar al-Assad.

XS
SM
MD
LG