Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 07:47

Tetemeko la ardhi Japan laangusha treni na kuharibu majumba

Tetemeko la ardhi limeharibu barabara iliyoko kati ya Kunimi IC na Shiroishi IC katika njia kuu ya Tohoku Expressway (tabaka ya chini) huko mjini Shiroishi, jimbo la Miyagi. (Photo by Handout / NEXCO East Nippon Expressway Company Limited / AFP)

Watu wanne wanaripotiwa kufariki na zaidi ya 100 kujeruhiwa nchini Japan baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea katika sehemu nyingi za pwani mashariki mwa nchi.

Maafisa wameonya kwamba tetemeko hilo huenda likasababisha Tsunami.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.4 kwa kipimo cha rikta limepiga sehemu za pwani ya Fukushima na kusababisha ajali ya treni ya mwendo kasi, barabara kupasuka na bidhaa kutapakaa madukani.

Mitetemao midogo midogo imeendelea kuripotiwa katika sehemu hiyo.

Tetemeko hilo limetokea siku chache baada ya Japan kuadhimisha miaka 11 baada ya kutokea tetemeko kubwa lililosababisha Tsunami na kuvuja kwa kinu cha nuclear katika sehemu hiyo.

Zaidi ya nyumba za watu 37,000 zimekosa umeme katika sehemu ambazo zimeathirika zaidi za Fukushima na Miyagi.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari

XS
SM
MD
LG