Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:56

Tanzia ya McCain : Ulimwengu wasubiri kusikia kutoka kwa Bush, Obama


Jeneza la Senata John McCain likiwa ndani ya Jengo la Bunge la Marekani, Aug. 31, 2018.
Jeneza la Senata John McCain likiwa ndani ya Jengo la Bunge la Marekani, Aug. 31, 2018.

Marais wastaafu wawili wa Marekani watatoa salamu za tanzia Jumamosi katika ibada ya kumbukumbu katika kanisa la Washington National Cathedral kwa ajili ya kumuenzi Seneta wa Arizona, aliyetumikia wadhifa huo kwa muda mrefu, John McCain.

George W. Bush wa chama cha Republikan na Barack Obama wa chama cha Demokrat watatoa wasifu wa rafiki yao katika ibada ambayo tayari ilikuwa imeandaliwa na McCain wakati alipokuwa akipambana na maradhi ya saratani.

McCain alipoteza nafasi ya kuwa rais alipochuana na Bush mwaka 2000 na baadae kushindwa tena katika kinyang’anyiro cha urais akichuana na Obama mwaka 2008.

Mwili wa McCain umewekwa ndani ya jengo la Bunge la Marekani Ijumaa. Mke wa McCain, Cindy, watoto wake saba na mama yake mwenye umri wa miaka 106, pamoja na wajumbe wa bunge la marekani walihudhuria hafla ya kumuenzi McCain Ijumaa katika ukumbi wa Rotunda, mjini Washington.

Seneta McCain ambaye aliwahi kushikiliwa nchini Vietnam kama mfungwa wa kivita na baadae maishani kugombea nafasi ya urais wa Marekani mara mbili amepewa heshima ya mwili wake kuwekwa ndani ya jengo la Bunge la Marekani kuanzia Ijumaa, siku mbili kabla ya kuzikwa.

McCain ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 81 atakumbukwa kwa uwezo wake wakufikia kambi ya upinzani.

XS
SM
MD
LG