Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:06

Tanzania yazuia mtu, NGOs kufungua kesi dhidi yake Mahakama ya Afrika


Serikali ya Tanzania imeondoa haki ya mtu na asasi za kiraia (NGOs) kuweza kufungua mashtaka dhidi yake katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Mataifa, Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limegundua.

Kuondolewa kwa haki hizi kutawanyang’anya watu na asasi mbalimbali nchini Tanzania nafasi muhimu ya kudai haki zao, katika nchi ambapo mfumo wake wa sheria umeharibika sana.

Tanzania ambayo iliwasilisha tamko hilo katika mahakama hiyo Novemba 14, 2019, ni nchi ya pili baada ya Rwanda, kuondoa haki ya watu na asasi za kiraia kuweza kuifikia mahakama ya Afrika, chombo muhimu cha kisheria cha bara la Afrika katika hali ambapo serikali inaingilia mifumo ya mahakama ya kitaifa.

Serikali ya Tanzania ina idadi kubwa ya kesi zilizo funguliwa na watu binafsi na asasi za kiraia na pia hukumu zilizotolewa dhidi yake na Mahakama hiyo ya Afrika.

Kati ya hukumu 70 zilizotolewa na Mahakama hiyo hadi mwezi Septemba 2019, hukumu 28, au asilimia 40, zilikuwa za Tanzania.

Hivyo hivyo, kesi nyingi kati ya hizo ambazo hazijatolewa hukumu mbele ya mahakama ya Afrika ni dhidi ya Tanzania, idadi kubwa ya hizo ni madai ya ukandamizaji wa haki ya mtu kufanyiwa uadilifu katika kutolewa hukumu, ikieleza kuwepo tatizo katika mfumo mzima wa mahakama nchini Tanzania.

Hivi karibuni, mnamo Novemba 28, Mahakama ya Afrika ilitoa hukumu kwamba kifungu cha adhabu ya jinai kinahalalisha adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji siyo tu kinakiuka haki ya mtu kuhukumiwa kwa uadilifu na kukandamiza uhuru wa mahakama, lakini pia haki ya mtu kuishi.

“Kesi nyingi zilizofunguliwa dhidi ya Tanzania katika mahakama ya Afrika zinaeleza hali ya kusikitisha ya nchi kushindwa kuwapa fidia za kutosha na zinazolingana na dhulma waliofanyiwa, kinyume cha haki za kibinadamu, amesema Japhet Biegon.

“Akiwa ni mwenyeji wa mahakama ya Afrika, Tanzania inatakiwa kuongoza kwa mfano na itafakari upya uamuzi wake huo, na kuondoa tamko la kuondoa haki ya mtu na asasi za kiraia, na ionyeshe kuunga kwake mkono na azma ya kuona kwamba mahakama hiyo ya Afrika inafanikiwa.Ni lazima iimarishe mfumo wa mahakama zake kuhakikisha kuwa wale wote waliodhulumiwa haki zao wanapata fursa ya kusikilizwa na mahakama katika ngazi ya kitaifa.”

XS
SM
MD
LG