Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:44

Tanzania yatahadharisha juu ya kura ya maoni Burundi


Wafuasi wa chama tawala cha Burundi - CNDD-FDD), wakidansi katika mkutano wao wa mwisho kabla ya kura za maoni kupigwa Bujumbura, Burundi, Mei 14, 2018.
Wafuasi wa chama tawala cha Burundi - CNDD-FDD), wakidansi katika mkutano wao wa mwisho kabla ya kura za maoni kupigwa Bujumbura, Burundi, Mei 14, 2018.

Tanzania imeeleza wasiwasi wake juu ya hatua ya Burundi kuitisha kura ya maoni jambo linalopingwa vikali ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Augustine Mahiga ametahadharisha kuwa kura hiyo ya maoni inaweza kuharibu mazungumzo ya usuluhishi yanayoendelea hivi sasa baina ya serikali na vyama vya upinzani.

Wananchi wa Burundi wanajiandaa kesho Alhamisi kupiga kura ya maoni ambayo kama itapitishwa na kuwa sheria itamruhsu Rais aliyoko madarakani Piere Nkurunzinza kuendelea kutawala hadi mwaka 2034.

Mazungumzo ya kutafuta suluhu nchini humo tangu kuzuka vurugu baada ya Rais Nkurunzinza kugombea urais kwa awamu ya tatu yameleta mvutano mkubwa baina ya pande hizo mbili hasimu.

Wakati kampeni za kura ya maoni itakayofanyika tareh 17 Mei zikiendelea, vyama vya upinzani nchini humo vimelalamikia hatua hiyo na kudai kuwa ni kinyume cha katiba.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Burundi watu kadhaa wameripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kushawishi wananchi kususia kushiriki katika zoezi hilo la kupiga kura.

XS
SM
MD
LG