Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:34

Tanzania: Watu 12 wafariki katika Ajali ya basi la abiria, 63 wajeruhiwa


Ajali ya barabarani nchini Tanzania. Picha kwa hisani ya Global Publishers Tanzania
Ajali ya barabarani nchini Tanzania. Picha kwa hisani ya Global Publishers Tanzania

Watu 12 wamefariki dunia na wengine 63  wamejeruhiwa baada ya basi la abiria  la kampuni ya  Frester lililokuwa likisafiri kutokea  Bukoba kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori lililokuwa na  shehena ya  saruji.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia tarehe 9 Februari katika maeneo ya kijiji cha Silwa Pandambili, kilichopo barabara kuu inayotoka Dodoma kwenda Morogoro.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyonukuliwa na Global Publishers, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Kulingana na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dkt Ernest Ibenzi majeruhi 15 wa ajali hiyo wamefikikshwa katika hospitali hiyo.

Amesema wanaendelea kuwapatiwa matibabu na wale watakaopata nafuu watawaruhusu kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remidius Mwema majeruhi wa ajali hiyo ni 63, wanaume 40 wanawake 23.

Majeruhi 36 wapo katika hospitali ya wilaya ya Gairo, majeruhi 27 walipelekwa katika kituo cha Afya cha Kibaigwa ambapo kati ya hao 16 walihamishiwa hospitali ya wilaya ya Kongwa kwa matibabu zaidi na wengine walipelekwa Dodoma kutokana na hali zao kuwa siyo nzuri.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali nchini Tanzania.

XS
SM
MD
LG