Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:33

Wanane wafikishwa mahakamani kwa rushwa Tanzania.


Tiagi Masamaki aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA Tanzania afikishwa mahakamani.
Tiagi Masamaki aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA Tanzania afikishwa mahakamani.

Watu wanane kati ya 12 waliokuwa wakishikiliwa na kuhojiwa na polisi nchini Tanzania kutokana na kashfa ya upotevu wa makontena 329 pamoja na ukwepaji ushuru zaidi ya shillingi billion 80 wamepandishwa kizimbani katika mahakama moja ya mjini Dar es salaam leo.

Watuhumiwa hao 8 ikiwa ni pamoja na aliyekuwa kamishna wa forodha mamlaka ya mapato Tanzania TRA, Tiagi Masamaki, wanakabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kuhujumu uchumi pamoja na upotevu wa kiasi cha shilingi billion 12.7 na kuisababishia serikali ya Tanzania hasara.

Hii ni kesi ya kwanza ya madai ya rushwa kufikishwa mahakamani tangu serikali mpya ya Rais John Magufuli iliyoingia madarakami mwezi mmoja uliopita ianze kampeni ya kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma nchini humo

Kulingana na mashitaka hayo watuhumiwa walikula njama kutoa makontena kutoka bandari ya Dar es salaam na kuyapeleka katika bandari kavu ya kuhifadhiwa huku wakidai kuwa kontena hizo tayari zimelipiwa kodi

Katika shittaka la uhujumu uchumi washtakiwa wanatuhumiwa kuisababishia serikali hasara ya mabilion ya fedha kama mapato na kodi shitaka ambalo halina dhamana kwa kuwa mahakama ya Kisutu ambapo mashitaka hayo yamefunguliwa haina uwezo wa kisheria kusikiliza shauri hilo.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Harun Shaidi amesema upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuiahirisha kesi hiyo mpaka december 17 mwaka huu huku watuhumiwa wote wanane wakipelekwa rumande

Waliopaandshwa kizimbani pamoja na Tiagi Masamaki ni Habib Hamis -Meneja huduma na Wateja -TRA, Haroun Mapande Mkuu wa Mfumo wa ICT -TRA, Raymond Adolf Luice wa TRA, Eliachi Mrema Afisa wa TRA Katika bandari kavu ya Azam, AShraf Yusuph Khan meneja wa ICD ya Azam pamoja na Bolton Adolf Meneja udhibiti wa TRA.

XS
SM
MD
LG