Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 20:06

Tanzania inadaiwa shilingi Trilioni 91.02, deni linaongezeka kila mwezi kwa dola milioni 544


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Deni la serikali ya Tanzania linaendelea kuongezeka kila mwezi kwa kiasi cha dola milioni 544.8. Haya ni kulingana na ripoti ya benki kuu ya nchi hiyo - BoT.

Kufikia mwezi Oktoba 2022, Tanzania ilikuwa inadaiwa shilingi trilioni 64 ikiwa ni deni ambalo nchi hiyo inadaiwa na nchi au wafadhili wan je, ambayo ni asilimia 70.6 ya deni la jumla la serikali.

Wakopeshaji wa ndani wanadai serikali shilingi trilioni 26.6.

Sekta ya uchukuzi na mawasiliano inaongoza kwa kiasi kikubwa cha deni, zikifatiwa na huduma kwa jamii, elimu, nshati na madini.

Wakopeshaji wakuu wa ndani ya nchi ni kutoka kwa mfuko wa pensheni pamoja na benki za biashara, ikiwa inafikia kiwango cha asilimia 55.8 cha deni la jumla la serikali.

Kulingana na gazeti la The Citizen, waziri wa fedha na mipango Mwigulu Nchema, alisema mwezi Juni mwaka huu kwamba ongezeko la deni la serikali linatokana na kuongezeka kwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Serikali ya Tanzania imesema kwamba japo deni la linaendelea kuongezeka, ina uwezo wa kulipa.

XS
SM
MD
LG