Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 21:43

Sudan: Mapigano kati ya jeshi na vikosi vya wanamgambo yaendelea kwa siku ya tatu


moshi ukipaa angani kutoka katika lami ya kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Khartoum wakati moto ukiwaka, huko Khartoum
moshi ukipaa angani kutoka katika lami ya kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Khartoum wakati moto ukiwaka, huko Khartoum

Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Sudan Khartoum Jumatatu wakati mapigano kati ya jeshi na vikosi vya wanamgambo vinavyoongozwa na majenerali hasimu  yakiendelea kwa siku ya tatu huku idadi ya waliouwawa ikiongezeka kufikia karibu 100.

Ghasia zimezuka Jumamosi baada ya wiki kadhaa za mzozo wa kugombea madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua madaraka katika mapinduzi mwaka 2021, mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al –Burhan na naibu wake Mohamed Hamdam Daglo ambaye anaongoza kikosi cha usaidizi wa haraka cha wanamgambo RSF.

Mapigano makali yaliyojumuisha mashambulizi ya anga , vifaru mitaani, na silaha nzito katika maeneo yaliyo na watu wengi kwenye mji mkuu Khartoum na miji mingine kote sudan yamezua madai ya kimataifa kutaka sitisho la mapigano kufanyika haraka .

Moshi ukienea angani katika eneo la makazi ya watu huko Khartoum, April 16, 2023, wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya pili kati ya majenerali wawili mahasimu.
Moshi ukienea angani katika eneo la makazi ya watu huko Khartoum, April 16, 2023, wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya pili kati ya majenerali wawili mahasimu.

Umoja wa Afrika , jumuiya ya kiarabu, na nchi jirani ya Sudan – Misri, na Sudan kusini wametoa wito kwa pande zinazohasimiana kutafuta njia ya amani dhidi ya mzozo unaoendelea.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limefanya Mkutano wa dharura jumapili kuhusu hali ya sudan na kupinga hatua ya kuingiliwa kijeshi ambayo inaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi nchini Sudan. Jumuiya ya kiarabu nayo pia ilifanya Mkutano wake wa dharura mjini cairo , ambako wawakilishi wa nchi za kiarabu walijadiliana kuhusu mapigano yanayoendelea sudan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amelaani ghasia hizo nchini Sudan na kusema kuwa hatua kubwa zinatakiwa kuchukuliwa kuwalinda raia.

Waziri wa Mambo ya Nje amesema:“ Kuna wasiwasi mkubwa wa pamoja kuhusu mapigano , ghasia zinazoendelea nchini Sudan. Tishio linaloletwa kwa raia , linaloletwa kwa taifa la sudan na linaweza kuwa na athari hata katika eneo hilo.”

XS
SM
MD
LG