Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 02:35

Mapigano yamezuka Sudan kati ya jeshi na kikosi cha wanamgambo nchini Sudan


Ramani ya Sudan na nchi zinazopakana nao
Ramani ya Sudan na nchi zinazopakana nao

Mjini Khartoum sauti nzito za ufyatuaji risasi zilisikika katika maeneo kadhaa ikijumuisha katikati ya jiji na kitongoji cha Bahri. Katika mfululizo  wa taarifa wanamgambo wa Rapid Support Forces walilishutumu jeshi kwa kushambulia vikosi vyake katika moja ya kambi zake huko kusini mwa Khartoum

Mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na kikosi chenye nguvu cha wanamgambo nchini humo yalizuka Jumamosi katika mji mkuu na kwingineko katika taifa hilo la Afrika na kuzusha hofu ya kuzuka kwa mzozo mkubwa katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko.

Mjini Khartoum sauti nzito za ufyatuaji risasi zilisikika katika maeneo kadhaa ikijumuisha katikati ya jiji na kitongoji cha Bahri. Katika mfululizo wa taarifa wanamgambo wa Rapid Support Forces, walilishutumu jeshi kwa kushambulia vikosi vyake katika moja ya kambi zake huko kusini mwa Khartoum.

Walidai waliuteka uwanja wa ndege wa mji huo na kudhibiti kabisa Ikulu ya Jamhuri mjini Khartoum, makazi ya rais wa nchi hiyo. Kundi hilo pia limesema limeuteka uwanja wa ndege na kituo cha anga katika mji wa kaskazini wa Marawi, takribani kilomita 350 kaskazini magharibi mwa Khartoum.

Shirika la habari la Associated Press halikuweza kuthibitisha madai hayo. Jeshi la Sudan limesema mapigano yalizuka baada ya wanajeshi wa RSF kujaribu kushambulia vikosi vyake kusini mwa mji mkuu. Baadaye jeshi lilitangaza RSF kuwa kikosi cha waasi, ikielezea kauli za wanajeshi hao kama ni uongo.

XS
SM
MD
LG