Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 19:13

Sri Lanka: Mawaziri wote watajiuzulu, asema Waziri Mkuu

Waandamanaji waliovamia makazi ya Waziri Mkuu nchini Sri Lanka

Mtafaruku uliosababishwa na maandamano katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo, ambayo yamesababisha kujiuzulu kwa Rais Gotabaya Rajapaksa na Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe umeendelea hii leo, huku Waziri Mkuu akisema kwamba mawaziri wote watajiuzulu mara tu serikali ya mpito itakapoundwa.

Vyama vya upinzani vya Sri Lanka vilikutana Jumapili kujadili mchakato wa kuunda serikali mpya.

Mkutano huo ulifanyika siku moja baada ya rais na waziri mkuu kusema watajiuzulu. Lakini waandamanaji walisema wataendelea kuwepo katika makazi rasmi ya rais na waziri mkuu, mjini Colombo, hadi viongozi hao wawili watakapoondoka rasmi madarakani.

Maelfu ya waandamanaji walivamia nyumba ya Rais Rajapaksa na kuchoma moto makazi ya Waziri Mkuu Wickre-mesinghe, huku wakielezea hasira yao juu ya mgogoro wa kiuchumi ambao umdumu kwa miezi kadhaa.

Rajapaksa na waziri mkuu wamekubali kujiuzulu huku rais akimwambia spika wa bunge kuwa ataondoka Julai 13 ili kuhakikisha mpito mzuri wa madaraka. Hata hivyo, waandamanaji hao wanataka wajiuzulu mara moja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG