Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:14

Waandamanaji wa Sri Lanka waapa kuendelea kukalia makazi ya rais na waziri mkuu


Waandamanaji wakikusanyika ndani na karibu na majengo ya makazi rasmi ya waziri mkuu, July 10, 2022. Picha ya AP
Waandamanaji wakikusanyika ndani na karibu na majengo ya makazi rasmi ya waziri mkuu, July 10, 2022. Picha ya AP

Waandamanaji wa Sri Lanka Jumapili wamesema wataendelea kukalia makazi rasmi ya rais na waziri mkuu mjini Colombo hadi viongozi hao wawili watakapoondoka mamlakani rasmi .

Maelfu ya waandamanaji walivamia makazi hayo mawili Jumamosi. Walivamia nyumba ya Rais Rajapaksa na kuchoma makazi ya waziri mkuu Ranil Wickremesinghe wakati kukiwa hasira ya umma juu ya mzozo wa kiuchumi uliodumu kwa miezi kadhaa.

Kufuatia hayo, Rajapaksa na waziri mkuu walikubali kujiuzulu huku rais akimuelezea spika wa bunge kuwa ataondoka madarakani Julai 13 ili kuhakikisha kipindi cha mpito kinafanyika kwa usalama.

Hata hivyo, waandamanaji wanataka viongozi hao kujiuzulu mara moja.

Rais Rajapaksa alipelekwa na wanajeshi mahali salama, sehemu ambayo haikutangazwa kabla ya maandamano hayo makubwa.

Akilaumiwa sana kwa kuzorota kwa uchumi, rais alikuwa chini ya shinikizo la umma kujiuzulu kwa miezi kadhaa sasa.

XS
SM
MD
LG