Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:33

Somalia: Watu sita wafariki katika mlipuko uliolenga basi


FILE - Wakazi wakitathmini uhabifu uliosababishwa na shambulizi katika Hoteli ya Pearl Beach, Mogadishu Juni 10, 2023.
FILE - Wakazi wakitathmini uhabifu uliosababishwa na shambulizi katika Hoteli ya Pearl Beach, Mogadishu Juni 10, 2023.

Takriban watu sita wamekufa katika mlipuko uliolenga basi la abiria lililokuwa linasafiri katika mkoa nje ya mji mkuu wa Somalia Jumatano shirika la habari la serikali limesema.

Shirika la habari la Somalia limemnukuu Mohamed Ibrahim gavana wa Lower shabelle akisema kuwa shambulizi lilitokea katika barabara baina ya wilaya za Ooryoley na Marka na kwamba watu wengine 12 wamejeruhiwa.

Ibrahim amesema shambulizi la kigaidi limesababisha mlipuko , shirika hilo la habari limeandika katika mtandao wa X ambao awali ulikuwa unajulikana kama twitter.

Hata hivyo Ibrahim hakufafanua zaidi ni kundi gani lililotuhumiwa kufanya shambulizi . lakini kundi la wanamgambo la Al shabab lenye uhusiano na al qaida awali lilidai kuhusika na mashambulizi kama hayo.

Kundi hilo limekuwa likipigana tangu mwaka 2006 ili kutaka kuipindua serikali kuu ya somalia na kuweka sheria yake yenye msimamo mkali maarufu kama SHARIA.

Forum

XS
SM
MD
LG