Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:24

Wanajeshi kadhaa wameuawa Somalia baada ya kambi yao kushambuliwa na Al-shabaab


Wanajeshi wa Somalia

Watu kadhaa wanaripotiwa kufariki katika shambulizi la kujitoa mhanga kwenye kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Jaale Siyaad, mjini Mogadishu, Somalia.

Mshambuliaji aliwalenga maafisa wa jeshi walipokuwa wamejipanga foleni kupata kiamsha kinywa.

Afisa wa jeshi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu haruhusiwi kuzungumza na vyombo vya habari, ameiambia VOA kwamba wanajeshi 20 wamefariki, na Darzeni kujeruhiwa.

Baadhi ya wanajeshi walijeruhiwa vibaya sana na hali yao sio nzuri.

Kundi la kigaidi la Al-shabaab limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Katika ujumbe wake wa Telegram, kundi hilo limedai kwamba mmoja wa washambuliaji wake wa kujitoa mhanga aliwalenga wanajeshi hao.

Kundi la Al-shabaab limedai kwamba wanajeshi 73 wamefariki na 124 kujeruhiwa. Ripoti hizo hazijathibitishwa na vyombo huru.

Mlipuaji alikuwa amevalia sare ya kijeshi, na haijabainika namna alivyoingia kwenye kambi hiyo ya jeshi, ambayo ni mojawapo ya kambi zenye ulinzi mkali sana mjini Mogadishu.

Forum

XS
SM
MD
LG