Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:15

Baraza la Usalama litakutana kujadili jaribio la kombora la Iran


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana katika kikao chake cha dharura Jumanne kufuatia jaribio la kombora la ballistika lililofanywa na Iran.

Marekani imeitisha mkutano huo baada ya jaribio hilo la Iran Jumamosi. Hata hivyo haijajulikana ni kombora la aina gani na lina uwezo gani.

Azimio la Baraza la Usalama la 2015 linaikataza Iran kujihusisha na jaribio lolote la matumizi ya kombora la ballistika ambalo linauwezo wa kusafirisha vichwa vyenye silaha za nyuklia.

Kupigwa marufuku huko kunafuatia makubaliano kati ya nchi ya Iran na nchi sita zenye nguvu zinazokusudia kupunguza nguvu za programu yake ya nyuklia ikibadilishana na kulegezwa kwa vikwazo ilivyowekewa.

Makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, China na Ujerumani yalianzishwa baada ya kuwepo tuhuma za kuwa Iran ilikuwa inajiandaa kutengeneza silaha za Nyuklia, ambalo Iran wamekanusha mara nyingi.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Tehran Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje Mohammad Javad Zarif hakuthibitisha wala kukanusha kuwepo jaribio la kombora hilo, lakini alisisitiza kuwa msimamo wa Iran kuwa makombora yake hayana uwezo wa kubebe silaha za nyuklia uko pale pale.

Mchambuzi Muiran wa Chuo Kikuu cha Indiana Hussein Banai amesema anafikiri kuwa motisha uliyopelekea jaribio hilo la Irani ni kisiasa zaidi, na Iran imejifunza “wafanye nini kujibu ubabe wa uongozi wa Marekani.”

Rais Donald Trump amekuwa mkosoaji mkubwa wa makubaliano ya nyuklia ya Iran, akisema kuwa dunia imempa fursa kubwa Iran kujiimarisha kuliko kile waliweza kupata kutoka kwa uongozi wa Iran.

XS
SM
MD
LG