Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:37

Maelfu waandamana Marekani kupinga amri ya Rais Trump


Waandamanaji wakishikana mkono kuonesha umoja dhidi ya amri ya Rais Trump
Waandamanaji wakishikana mkono kuonesha umoja dhidi ya amri ya Rais Trump

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika Jumapili karibu na White House huko Washington DC kwa siku ya pili ya malalamiko katika miji mikubwa kote Marekani dhidi ya marufuku ya safari iliyotolewa na Rais Donald Trump kutoka nchi saba za kiislam.

Waandamanaji wakipiga kelele “Hakuna chuki, Hakuna Khofu, Wakimbizi wanakaribishwa hapa, waandamanaji waliishambulia amri ya Rais Trump ambayo inawazuia wakimbizi wote kuingia Marekani angalau kwa siku 120.

Amri hiyo pia inazuia viza kutoka raia wa Somalia, Sudan, Libya, Yemen, Iran na Irak kwa siku 90 na marufuku kama hiyo kwa raia wa Syria. Malalamiko yanafanyika hasa katika miji ya New York, Los Angeles, Philadelphia, Houston, Boston, Atlanta, Louisville na Detroit.

Watu kadhaa walishikiliwa kwa muda wa siku nzima Jumapili walipowasili Marekani kutoka baadhi ya nchi hizo na kuachiwa huru baada ya mahakama kuingilia kati.

XS
SM
MD
LG