Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 00:07

Mgomo Marekani: 'Siku bila ya mwanamke'


Maandamano ya siku ya wanawake duniani Washington.
Maandamano ya siku ya wanawake duniani Washington.

Kikundi kilichoandaa maadamano ya wanawake mwezi Januari mjini Washington kimewataka wanawake kuchukua mapumziko siku ya Jumatano ili kuonyesha umuhimu wao katika kuchangia uchumi wa taifa.

Tukio hilo lililoitwa “Siku bila ya Mwanamke,” limekusudiwa lioanishwe na siku ya Wanawake Duniani, na iweke wazi nafasi ya kiuchumi ya mwanamke aliyokuwa nayo; na hilo ni kwa kuwataka wakae nyumbani siku hiyo bila ya kufanya kazi na pia wasitumie pesa zao.

Mgomo huo wa wanawake ni ishara ya hatua kubwa ya kwanza iliochukuliwa na kundi hilo tangu Januari 21, wakati mamilioni ya watu walipojitokeza barabarani katika miji mbalimbali Marekani kuonyesha upinzani wao dhidi ya Rais Donald Trump alipoapishwa.

Trump alituma ujumbe wa Twitter Jumatano kuonyesha kuunga mkono siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo inatambuliwa na Umoja wa Mataifa. Lakini hakugusia kabisa mgomo huo.

Siku ya wanawake Dunia ni wakati wa kutafakari juu ya maendeleo ya wanawake, kutangaza mabadiliko na kusheherekea vitendo vya ujasiri na uthubutu vya wanawake wa kawaida ambao wamechukua majukumu yasiyo ya kawaida katika historia ya nchi zao na jamii pia.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: Wanawake katika ulimwengu wa ajira unaobadilika: Kufikia usawa (50-50) ulimwenguni ifikapo 2030.

Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa mwaka 1945; uliridhia Machi 8, kuwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo ulizingatia hali halisi kuwa, masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo wa pekee.

XS
SM
MD
LG