Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:30

Siku ya Kifua Kikuu Duniani: Madaktari waonya kuendelea kwa maambukizo sugu


Mario Raviglione
Mario Raviglione

Siku ya Kifua Kikuu Duniani, inalengo la kuongeza uelewa kuhusu maradhi ambayo kila siku watu 5,000 wamekuwa wakipoteza maisha.

TB inawaathiri zaidi makundi ya watu wanyonge wakiwemo wahamiaji, wakimbizi, wafungwa, watu ambao wanakandamizwa katika jamii,” amesema Mario Raviglione, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Programu ya Kimataifa ya Kifua Kikuu.

Maradhi ya TB yamekuwa yakiwaua takriban watu milioni 1.8 kila mwaka. Nchi sita zinachangia karibuni thuluthi mbili ya wagonjwa hao ikiwemo India, Indonesia, China, Nigeria, Pakistan na Afrika Kusini.

Ijumaa ni kumbukumbu ya siku ya mwaka 1882 wakati mwanasayansi wa Kijerumani Dr Robert Koch alipotangaza kwamba amegundua kile kinacho sababisha ugonjwa huo, ambavyo ni vimelea vya bacillus. Mpaka sasa bado ni moja ya maradhi hatari yenye kuambukiza ulimwenguni.

Kila siku watu 5,000 wanapoteza maisha kwa sababu ya ugonjwa wa kifua kikuu.

Maambukizo sugu

Katika miaka ya hivi karibuni matatizo ya maambukizo sugu ya TB yameongezeka duniani kutokana na dawa hizo kutokufanya kazi, na kuwa imeleta udharura juu ya ongezeko la tishio la afya ya jamii. Vimelea vya TB mara nyingi vinaweza kusambaa bila kujulikana katika jamii.

“Afrika Kusini, kwa mfano, TB ni kisababisho cha kawaida cha vifo na maradhi hayo yameshindikana kudhibitiwa Afrika,” amesema Dr Keertan Dheda, Mkuu wa kitengo cha matatizo ya mapafu katika Chuo Kikuu cha Cape Town.

Lakini kuna matumaini mapya wakati kiwango kidogo cha madawa aina mpya yameanza kupatikana.

“Kwa mara ya kwanza baada ya miongo minne hadi mitano, tumekuwa na madawa aina mbili. Aina moja ni bedaquiline,” Dheda amesema.

“Hivi sasa dawa hii imesajiliwa nchini Afrika Kusini na inapatikana kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa wengi ambao wamekuwa na TB sugu.

Na pia ipo dawa nyengine mpya inaitwa delamanid, ambayo bado haijapewa kibali huko South Afrika lakini inapatikana nchi nyingine.”

Dawa mpya lazima zitumiwe kwa uangalifu

Katika ripoti iliyochapishwa katika Jarida la Afya la Lancet, Dheda na mwandishi mwenza wameonya kuwa ubora wa dawa hizi katika kutibu inawezekana ikatoweka mara moja kama hazitumiwi inavyostahili.

“Kuna ripoti za hali za wagonjwa kadhaa ulimwenguni ambao tayari wamekuwa hawatibiki kwa dawa zote mbili delamanid na bedaquiline.

Tunahitaji kubadilisha mikakati yetu,” Dheda amesema.

“Tunahitaji kuikabili jamii na kuziibua hali hizi za wagonjwa. Ni lazima tushughulikie vichocheo vikuu vya TB, ikiwemo umaskini na kufurika kwa makundi ya watu, ukosefu wa lishe, utumiaji mbaya wa pombe, kuvuta hewa za sumu zinazotokana na sigara na kuchoma kuni,” Dheda ameongeza katika mahojiano yake na VOA Alhamisi.

Ripoti hiyo imeonya kuwa madawa mpya ni lazima zitolewe kwa kusudio la kutibu mtu moja moja pamoja na wagonjwa kupewa muongozo wa matumizi ilikuzuia tatizo la maambukizi sugu ya maradhi ya TB.

XS
SM
MD
LG