Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:29

Watu zaidi wakamatwa kufuatia shambulio la ugaidi London


Mishumaa iliyowashwa kuomboleza mauaji katika daraja la Westminster, London
Mishumaa iliyowashwa kuomboleza mauaji katika daraja la Westminster, London

Polisi London wamesema Ijumaa wanawashikilia watu wawili zaidi kuhusiana na shambulizi karibu na Bunge la Uingereza.

Kamanda mwenye kushughulikia kupambana na ugaidi Mark Rowley ameeleza ukamataji huo kama ni hatua “muhimu” japokuwa hakutoa maelezo zaidi. Amesema watu tisa tayari wako mbaroni na mtu mmoja ameachiwa.

Maafisa wa polisi wametambua mshambuliaji ambae amewaua watu wane karibu na Jengo la Bunge kama Khalid Masood, Muingereza ambae aliingia katika Uislam na alikuwa ana rikodi ya muda mrefu ya uhalifu kwa kumiliki silaha na tuhuma nyingine.

Rowley amesema jina la Masood la kuzaliwa ni Adrian Russell Ajao na ameomba watu kutoa taarifa zozote walizokuwa nazo kuhusu mtu huyu.

“Tunasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa mtu yoyote ambae anamjua Khalid Masood vizuri, anajua nani ni washirika wake na kutupa taarifa kuhusu sehemu ambazo hivi karibuni ametembelea,” Rowley amesema.

“Inawezekana kulikuwa na watu walikuwa na duku duku kuhusu Masood lakini hawakuwa wakijisikia vizuri kwa sababu yoyote kutoa malalamik yao kwetu.”

Kikundi cha Islamic State kimesema Masood, 52, alikuwa ni “askari” wa kikundi chenye siasa kali ambae aliitikia wito wao wa kuwashambulia raia na wanajeshi katika nchi ambazo zimeungana na Marekani katika kuitokomeza IS.

XS
SM
MD
LG