Ripoti mpya iliotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International inasema kuwa karibu watu 150 wakiwemo watoto 11 walio chini ya umri wa miaka 6 wamekufa mwaka huu wakiwa kwenye kizuizi cha jeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Shirika hilo limesema kuwa watoto hao wakiwemo wanne wachanga walikuwa miongoni mwa vifo 149 vya wafungwa vilvyoripotiwa kutokea kwenye kituo cha kijeshi cha Gawa maarufu kwa kuwazuia watu kilichoko kwenye mji wa Maiduguri na ambacho kimelalamikiwa siku zilizopita na vikundi vya kutetea haki.
Kituo hicho kinatumika kuwazauia washukiwa wa kundi la Boko Haram ambao kwa karibu miaka 8 wameuwa takriban watu 20,000 kaskazani mashariki mwa Nigeria.