Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:21

Serikali iliyopita ya Nigeria yashutumiwa kwa rushwa


Makamu rais wa Nigeria, Yemi Osinbajo.
Makamu rais wa Nigeria, Yemi Osinbajo.

Makamu Rais wa Nigeria anasema serikali iliyopita iliiba kiasi cha dola bilioni 15 fedha za umma kupitia mikataba ya kilaghai ya silaha.

Makamu Rais Yemi Osinbajo alisema leo Jumanne kwamba fedha hizo zilipotea kupitia vitendo vya rushwa katika matumizi ya vifaa vya usalama wakati wa utawala wa Rais wa zamani Goodluck Jonathan.

Rais aliyeko sasa madarakani Muhammadu Buhari aliyeshinda uchaguzi wa mwaka uliopita aliahidi kukabiliana na matatizo sugu ya rushwa. Buhari anasema wizi wakati wa utawala wa Jonathan umeiacha mifuko ya serikali ikiwa haina fedha kabisa. Tangu achukue madaraka mwezi Mei mwaka jana, maafisa kadhaa wa zamani wamekamatwa kwa mashtaka ya rushwa akiwemo mshauri wa zamani wa usalama wa taifa, sambo Dusuki.

XS
SM
MD
LG