Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 04:07

Nigeria yawakumbuka wasichana wa Chibok

Watu wakiwa wameshika mishumaa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutekwa kwa wasichana wanafunzi kutoka shule za sekondari ya Chibok nchini Nigeria.
Watu wakiwa wameshika mishumaa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutekwa kwa wasichana wanafunzi kutoka shule za sekondari ya Chibok nchini Nigeria.

Miaka miwili baada ya kutekwa wasichana zaidi ya 200 kaskazini mwa Nigeria na kundi la Boko Haram, video mpya inayoonyesha wasichana hao waliopotea ikiwa ni miezi minne tu iliyopita imewapa wazazi matumaini kwamba watoto wao bado wako hai.

Chibok girls 2nd year anniversary rally in Abuja, Nigeria April 14, 2016
Chibok girls 2nd year anniversary rally in Abuja, Nigeria April 14, 2016

Mpaka sasa kumekuwa hakuna habari yeyote juu ya wasichana hao 219 waliotekwa na Boko Haram 2014 kutoka shule moja katika mji wa Chibok jambo ambalo lilipelekea shutuma ya ulimwengu mzima, maandamano ya mitaani nchini Nigeria na watu wakijitolea kusaidia kuwatafuta kutoka nchi washirika.

Video mpya iliyoonekana Jumatano ambayo inaonyesha wasichana 15 kati yao na huenda imechukuliwa mwezi Desemba, hiyo ni alama ya kwanza ya waliotekwa tangu walipoonekana kwenye video ya Boko Haram ya propaganda muda mfupi baada ya kutekwa.

XS
SM
MD
LG