Watu wamepokea sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya mihamala ya kieletroniki kwa hisia tofauti kupitia mitandao mbalimbali.
Sheria hizo zilizoanza rasmi tarehe Mosi ya mwezi Septemba mwaka huu wa 2015, imeonekana kuwa na mapokezi chanya na hasi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Baadhi ya watu waliounga mkono sheria hiyo walikuwa na haya ya kusema kutoka kwenye mtandao wa Twitter.
Pamoja na hayo, lakini wapo wale ambao hawakuonesha kufurahishwa, na pengine walitoa maoni yao kwa kuzingatia kwamba wanaweza wakawa watu wa kwanza kukumbwa na sheria hizo.
Unaweza kuendelea na mjadala wa sheria hizi ambazo wadau wa haki na uhuru wa kutoa na kupokea maoni wamekuwa na hisia tofauti.